Tuesday, 17 January 2017

FAHAMU DAWA TANO ASILIA ZA KUONDOA CHUNUSI.

1.LIMAO.
Limao hujulikana kwa weng kama kiungo cha kuleta radha katika mboga, lakini kwa Upande mwingine , Limao ni dawa asilia  ambayo huondoa chunusi katika ngozi  .Jinsi yakutumia; Chukua Limao kisha likate katika vipande Viwili, halafu likamue Limao lako  kisha Chukua maji ya Limao hilo na kuyapaka katika eneo/sehemu ambayo Ina chunusi, na uiache kwa muda wa dakika (5-10),
Baada ya hapo uoshe USO
 wako kwa maji safi Yenye uvuguvugu.
2.ASALI.
Hii pia ni dawa  asilia kabisa ya kuondoa chunusi katika ngozi,ijapokuwa Asali imekuwa ni dawa inayotibu magonjwa  mbalimbali.Jinsi ya kutumia;
Weka asali kidogo kwenye sehemu ambayo ina chunusi, na uiache ifanye kazi kwa mdawa dakika (10-15), Kisha osha uso wako kwa maji yenye  uvuguvugu.
3.PAPAI.
Hili ni tunda, ambayo watu wengi huwa hawajagundua kuwa tunda hilo pia n dawa asilia kabisa ambayo ina  mchango makubwa kuondoa chunusi katika ngozi. Jinsi ya kufanya;Chukua kipande cha papai na kisha ponda  ponda vipande vidogo vidogo,kisha Chukua vipande hivo  vilivyopondwa kisha vipake kwenye sehemu ambayo kuna chunusi, Iache dawa hiyo ifanye kazi kwa mda Wa dakika (5-10), baada ya hapo osha uso wako kwa maji ya kawaida.
4.DAWA YA MENO.
Dawa ya meno, kama tunavyofahamu wengi wetu ni kwamba katika dawa ya meno huwa kuna kemikali ambazo huua bacteria katika meno, vivo hivo katika kuondoa pia chunusi katika ngozi, lakini so kila dawa ya meno,inauwezo wa kuondoa chunusi, lakini hii ni kwa zile dawa za meno ambazo ni (non-gel) tuu, ndo zenye uwezo wa  kuondoa chunusi.
5.PODA.
Ijapokuwa poda ni moja ya Urembo, lakini pia kwa Upande mwingine poda hutumika kama dawa ya kuondoa chunusi usoni.Lakini si kila pods inao uwezo wa kuondoa chunusi ,Unashauriwa kupaka baby powder usiku na Kuniacha hadi asubuhi.Ukifanya hivo mara kwa Mara utaufanya uso  wako kuondokana na chunusi.

Kwa Leo naomba niishie hapo, Lakini nakushauri tuu kwa wewe ambae ulikuwa unasumbuliwa kwa mda mrefu na chunusi, na Huenda ulikuwa bado hujapata dawa asilia za kuondoa chunusi , naomba zingatia maelekezo ya DAWA hizo hapo juu, kisha utajionea mwenyew Matokeo mazuri ya ngozi yako.

No comments:

Post a Comment